TANZIA: CHARLES HILARY AFARIKI DUNIA


Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary, amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Charles pia aliwahi kuwa mtumishi mwandamizi wa Azam Media Limited kati ya mwaka 2015 na 2023. Alihitimisha muda wake akiwa Mkuu wa Idara ya redio ya UFM, baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu, Hilary amefariki baada ya kuugua ghafla na mauti yamemkuta akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila.

Mtangazaji huyo wa zamani kinara wa Azam News na Mkuu wa UFM Redio ana historia ndefu katika utangazaji akiwa amevitumikia vituo mbalimbali vya habari ikiwemo Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati huo ikiitwa Redio Tanzania na Shirika la Utangazaji wa Uingereza (BBC) na DW Idhaa ya Kiswahili.

Pumzika kwa amani Legendary 

#R.I.P
#mpembatv📺
#mpembapic📸

Comments