PEP GUARDIOLA amepoteza mechi ya TANO mfululizo kwa mara ya kwanza akiwa meneja wakati Tottenham ilipoisambaratisha Manchester City 4-0 leo huko Etihad.
Baada ya presha ya mapema ya City, Maddison aliipatia Spurs bao la kuongoza akipokea pasi safi ya Dejan Kulusevski,
Na mchezaji huyo wa Uingereza alipata goli lingine katika dakika ya 20 na magoli mengine yakifungwa na Pedro Porro dakika ya 52 akipokea pasi safi kutoka kwa Solanke na Brennan Johnson aliyekamilisha kipigo hicho cha goli nne kwa City dakika ya 90.
Kwa hali ilivyo, Liverpool wanaweza kusonga mbele kwa pointi nane juu ya City kwenye kilele ikiwa watashinda dhidi ya Southampton Jumapili.




Comments
Post a Comment