"Nilipotua Tanzania nilimkuta kocha Gamondi tukafanya mazungumzo na Viongozi wa Timu tukakubaliana na viongozi. Baada ya hapo nikaona mambo mengi kupitia mitandao ya kijamii ikinionyesha mimi ni kocha mbovu kabisa Yanga wamejichanganya. Mkalimani alinionyesha mengi sana mitandaoni lakini Rais wa klabu alinifuata na kuniambia wewe onyesha utaalamu wako utawaona haohao watakuimba.
Kweli nilipata ushirikiano wote toka kwa Uongozi nikafanikiwa kutoa nilichotoa kwa asilimia kubwa tu.
Leo nmeondoka wanalaumiwa tena viongozi ndo nikakumbuka maneno ya Rais.
Aidha hawa watu hawajui kazi zao ama wanafanya kazi kwa uchochezi au ushamba.
Pale Yanga wana falsafa zao ambazo nilizikuta na sikusumbuka kabisa kila kitu nilipewa kuanzia Jina nikaitwa GERMAN MASHINE kama mnakumbuka press yangu niliwaambia niitwe Tanzania Mashine.
Wakaniletea falsafa ya GUSA ACHIA TWENDE KWAO ikaimbwa nikatembea nayo ikatiki.
Naomba niwatoe hofu mashabiki wa Yanga,Pale wana wachezaji High class kocha yeyote akipewa ushirikiano kama wangu atafanya vizuri sana.
Hizi kelele zingine ndo zile walizokuwa wanawaambia mimi nitawashusha daraja.Msikubali kuyumbishwa
Kwa heri WANANCHI tutaonana tena"
π£SEAD RAMOVIC Aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga

Comments
Post a Comment