Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa onyo kali kwa wananchi kutofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 24, 2025, wakati Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu, atakapofikishwa kwa ajili ya kesi ya uhaini inayomkabili.
Akizungumza Aprili 17, 2025 jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro, amesema jeshi hilo limefuatilia kwa kina mipango ya CHADEMA na kubaini uwezekano wa kutokea kwa vurugu ili kushinikiza vyombo vya sheria kumwachia Lissu, akisisitiza kuwa jeshi hilo halitaruhusu hilo litokee.
Onyo hilo limekuja baada ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA bara, John Heche, kutoa wito kwa wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi mahakamani Aprili 24, wakati Lissu atakaposomewa mashtaka.
#chadema
#mpembapic📸
#mpembatv📺
#KilaShowNiSafari

Comments
Post a Comment