▪️Papa akifa huchukuliwa pete yake na kupondwa maana Kanisa haliongozwi na aliyekufa, Ifahamike tu kuwa tangu Mwanzo pete zilivaliwa kuonyesha Mamlaka mfano Mfalme Daudi, Yosefu walivaa na wengine wengi tu, tuendelee.
▪️Baada ya PAPA kufa KARDINALI SHEMASI MKUU hushika nafasi ya Papa na kuitisha Semina ya Makardinali kuanzia siku 3 au zaidi pia huita watu wanaolifahamu Kanisa Katoliki vizuri ndani na nje hao wanawaambia Makardinali yoote kuhusu Ukatoliki.
▪️Wakimaliza ndipo unafanyika uchaguzi kwa kuwaapisha wote kutumia KANUNI YA IMANI, Baadaye wasiohusika hutolewa yaani waandishi wa habari na Markadinali wenye umri zaidi ya 80.
▪️Baadaye kura hupigwa ndani ya chumba yaani CONCLAVE wakati huo huandaliwa Viatu,kanzu na pete za saizi zote pamoja na mkanda kwaajili ya Papa atayechaguliwa, huandaliwa kwa saizi tofauti sababu haijulikani Papa atayechaguliwa atakuwa na saizi gani?
▪️Baadaye kura hupigwa kwa kuandika jina la kardinali anayefaa kuwa Papa mwenye kura 80 kati ya 120, kama kura hazijatimia basi kura hizo huchukuliwa na kuchomwa moto moshi mweusi hutoka kuashiria bado Papa hajapatikana (zoezi hili hufanyika raundi tatu kwa siku na kama hajapatikana bado Makardinali hukaa hata miezi 3 wakiendelea kuchagua mpaka apatikane)
▪️Akipatikana wanamuuliza unaona kura zimekuangukia UKO TAYARI? akikubali ndipo kura huchomwa na kemikali ya moto kuashiria TUMEMPATA PAPA.
▪️Hapo Kardinali Shemasi Mkuu huchungulia dirishani na kusema “TUNAYE PAPA”, Papa huvaa kila kitu cheupe maana rangi hiyo huonyesha UTAKATIFU.
▪️Baadaye Papa huulizwa utatuongoza kwa kufuata Utaratibu wa Mtakatifu nani? Akichagua Mwinjili YOHANE na Mtume PAULO basi Papa huyo ataitwa YOHANE PAULO na kama kuna Papa Mwingine tayari alishachagua majina hayo basi ataitwa YOHANE PAULO 1 na kama tayari kuna mapapa wawili walishachagua majina hayo basi huitwa YOHANE PAULO wa II, Papa wa sasa alipenda kufuata utaratibu wa Mtakatifu Fransisko wa Asizi yaani UPENDO, AMANI NA SALAMA ndio maana anaitwa Papa Fransisko
#mpembatv📺
#KilaShowNiSafari

Very nice
ReplyDelete