SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAJIVUNIA MAFANIKIO LUKUKI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA UONGOZI WA RAIS MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka minne imepata mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali.


Amesema mafanikio haya yanatokana na azma ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuujenga Utumishi wa Umma kuwa wenye tija katika maendeleo ya taifa.

Mhe. Simbachawene ameyasema hayo leo tarehe 17 Aprili, 2025 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO Jijini Dodoma.

Ameyataja miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana kuwa ni pamoja nakusimamia Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini ambapo Serikali ilijenga mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma (e-UTENDAJI - PEPMIS/PIPMIS) unaotumika kusimamia utendaji kazi wa watumishi wa umma na taasisi za umma ili kuwezesha kubaini kiwango cha utendaji kazi na uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma.

#mpembapic📸
#mpembatv📺
#KilaShowNiSafari 

Comments