YAO KOUASSI AFANYIWA UPASUAJI WA KIFUNDO CHA MGUU


Mlinzi wa kati wa Young Africans SC na timu ya taifa ya Ivory Coast, Attohoula Yao Kouassi, amefanyiwa upasuaji wa ligamenti ya kifundo cha mguu huko Tunis, Tunisia.

Kouassi alikuwa nje ya uwanja kwa muda sasa kutokana na jeraha hilo, na upasuaji huo ni hatua muhimu kuelekea urejeo wake uwanjani kwa ajili ya msimu ujao*.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu, mchezaji huyo anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi baada ya hatua za mwanzo za kupona kukamilika.

#mpembapic📸 

#mpembatv_3📺

#KilaShowNiSafari 

Comments