LAMINE YAMAL AWAPANIA URENO JUMAPILI

 

Nyota wa Uhispania Lamine Yamal amesema fainali ya Ligi ya Mataifa ya Jumapili dhidi ya Ureno itampa nafasi ya "kuthibitisha mimi ni nani" baada ya kuisaidia timu yake kuifunga Ufaransa katika nusu fainali siku ya Alhamisi.

Yamal alifunga mabao mawili na kutajwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika ushindi wa 5-4 dhidi ya Wafaransa hao mjini Stuttgart siku ya jana Alhamisi, na kutinga fainali ya Nations League.

"Ni mchezo maalum, fainali dhidi ya timu kubwa inatupa motisha ya ziada," Yamal aliwaambia wanahabari.

"Hii ndiyo aina ya mchezo ninaotaka kucheza, kuthibitisha mimi ni nani."

Akiwa bado na umri wa miaka 17, Yamal atamenyana na mkongwe wa Ureno Cristiano Ronaldo, ambaye ni mkubwa kwake kwa miaka 23.

"Yeye ni gwiji wa soka," Yamal alisema.

"Mimi, kama wachezaji wote, nina heshima kubwa kwa Cristiano.

"Nitafanya kazi yangu, ambayo ni kujaribu kushinda, na ndivyo hivyo," aliongeza.

Kocha wa Uhispania Luis de la Fuente alisema mashabiki wangeona "timu mbili zenye nguvu sana" Jumapili, na kuongeza "hii inaweza kuwa fainali ya Kombe la Dunia.

"Tunacheza dhidi ya mmoja wa magwiji: Cristiano Ronaldo. Jina lake pekee ndilo linalonitambulisha - ninavutiwa naye bila kikomo.

"Inapendeza sana kuona mchezaji katika umri wake akiendelea kucheza na kuwa fiti jinsi alivyo. Ninamkubali sana."

Mikel Merino, mfungaji mwingine wa Uhispania siku ya Alhamisi, alizungumza.

"Sio fainali yetu ya kwanza," alisema.

"Munich inatuletea kumbukumbu za kushangaza kutoka kwa Mashindano ya Uropa.

"Nina furaha sana kuwa katika fainali nyingine ni mafanikio makubwa na tunatumai tunaweza kushinda tena."

#mpembapic📸 

#mpembatv📺 

#KilaShoNiSafari 

#uefanationsleague 

#spain 

#lamineyamal 

Comments