Katibu wa Bunge, Ndg. Baraka Leonard ametangaza matokeo ya uthibitisho wa Waziri Mkuu ambapo amesema Waheshimiwa Wabunge wamemthibitisha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu kwa kura za Ndio 369.
Mbunge huyo wa Iramba Magharibi aliteuliwa na Mhe. Rais kuwa Waziri Mkuu na baadae uteuzi wake uliwasilishwa Bungeni kwa ajili ya kumthibitisha wakati wa Kikao cha Tatu cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 13 unaofanyika leo Novemba 13, 2025 Jijini Dodoma.

Comments
Post a Comment