MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI HAMZA JOHARI AAPISHWA KUWA MBUNGE

 Dodoma, 11 Novemba 2025 – Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari, amekula kiapo cha uaminifu mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Musa A. Zungu, katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge.

Kiapo hicho kimefanyika leo tarehe 11 Novemba 2025, ikiwa ni hatua muhimu inayompa Mhe. Johari hadhi ya kushiriki rasmi katika shughuli za Bunge kama Mbunge. Uapisho huo umefanyika kwa mujibu wa Ibara ya 59(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inampa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mamlaka ya kuwa Mbunge na kuhudhuria vikao vya Bunge bila ya kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi.

Hatua hii inaendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Bunge, hususan katika masuala ya ushauri wa kisheria, uundaji wa sheria, na utekelezaji wa majukumu ya kikatiba.

Kwa mujibu wa Katiba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni miongoni mwa maafisa waandamizi wa Serikali wanaoshiriki moja kwa moja katika mchakato wa kutunga sheria na kutoa tafsiri ya kisheria kwa taasisi za umma.ma, 11 Novemba 2025 – Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari, amekula kiapo cha uaminifu mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Musa A. Zungu, katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge.

Kiapo hicho kimefanyika leo tarehe 11 Novemba 2025, ikiwa ni hatua muhimu inayompa Mhe. Johari hadhi ya kushiriki rasmi katika shughuli za Bunge kama Mbunge. Uapisho huo umefanyika kwa mujibu wa Ibara ya 59(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inampa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mamlaka ya kuwa Mbunge na kuhudhuria vikao vya Bunge bila ya kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi.

Hatua hii inaendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Bunge, hususan katika masuala ya ushauri wa kisheria, uundaji wa sheria, na utekelezaji wa majukumu ya kikatiba.

Kwa mujibu wa Katiba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni miongoni mwa maafisa waandamizi wa Serikali wanaoshiriki moja kwa moja katika mchakato wa kutunga sheria na kutoa tafsiri ya kisheria kwa taasisi za umma.

Comments