NECTA WATANGAZA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2025

 


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Prof. Said A. Mohamed, ametangaza rasmi Matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2025 tarehe 5 Novemba 2025, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Baraza hilo, jumla ya watahiniwa 937,581, sawa na asilimia 81.80 ya watahiniwa 1,146,164 waliopata matokeo, wamefaulu mtihani huo na hivyo kustahili kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2026.

Mtihani wa Darasa la Saba 2025 (PSLE 2025) ulifanyika kati ya tarehe 10 hadi 11 Septemba 2025, ukihusisha shule za umma na binafsi katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Matokeo haya yanadhihirisha jitihada kubwa zinazofanywa na walimu, wazazi na wanafunzi katika kuinua kiwango cha elimu ya msingi nchini.

BONYEZA HAPA KUONA MATOKEO YA DARASA LA SABA

Comments

Post a Comment