Watu watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kupanga kufanya vurugu na kutaka kuchoma moto sehemu mbalimbali ikiwemo ofisi na makazi ya viongozi wa serikali, vituo vya Mafuta, yadi za mabasi zilizopo Tabora mjini siku ya uchaguzi mkuu 29/10/2025.
Hata hivyo watuhumiwa hao watano ambao kwasasa wote wapo mikononi mwa jeshi la polisi muda wowote kuanzia sasa watafikishwa Mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Comments
Post a Comment